WATU 15 WAFARIKI BAADA YA FERI KUZAMA UFILIPINO
Wafanyakazi wa uokoaji wameokoa watu 316 waliokuwa ndani ya meli ya MV Trisha Kerstin 3
Watu wasiopungua 15 wamefariki baada ya feri iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 350 na wafanyakazi wake kuzama kwenye maji ya pwani ya kusini mwa Ufilipino.
Wafanyakazi wa uokoaji wamewaokoa watu 316 waliokuwa ndani ya meli ya MV Trisha Kerstin 3, lakini watu 28 bado hawajulikani walipo.
Meli hiyo, ambayo ilikuwa ya mizigo na abiria, ilikuwa njiani kutoka kusini mwa nchi, Mindanao, kwenda kisiwa cha Jolo kusini-magharibi siku ya Jumatatu.
Serikali inasema wanachunguza chanzo cha kuzama.
Ufilipino - taifa la visiwa 7,100 - lina historia ndefu ya majanga ya baharini yanayohusisha feri.
Mei 2023, watu 28 walifariki baada ya kivuko cha abiria kushika moto. Waliofariki ni pamoja na watoto watatu, miongoni mwao mtoto wa miezi sita.