Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KIONGOZI WA UPINZANI UGANDA, KIZZA BESIGYE AKIMBIZWA HOSPITALINI

KIONGOZI WA UPINZANI UGANDA, KIZZA BESIGYE AKIMBIZWA HOSPITALINI

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, amekimbizwa katika hospitali ya Bugolobi baada ya hali yake ya kiafya kuzorota akiwa mahabusu katika Gereza la Luzira.

Maafisa wamesema Besigye alihamishwa usiku wa kuamkia Jumanne chini ya ulinzi mkali na kwa sasa yuko katika hali tete.

Chama chake, People's Front for Freedom, kimeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu afya yake na kimeitaka serikali kutoa uwazi juu ya matibabu anayopokea.

Besigye, ambaye ni kanali mstaafu na mgombea urais mara nne, amekuwa kizuizini tangu Novemba 2024 akikabiliwa na mashitaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, uhaini, na kuficha njama za uhaini.

Mawakili wa serikali wanadai alishirikiana na washirika kupanga kuipindua serikali ya Uganda kwa nguvu, kupitia mikutano iliyofanyika Nairobi, Geneva, Athens na Kampala.

Hali yake ya sasa imezua taharuki na kuongeza shinikizo kutoka kwa wapinzani na makundi ya haki za binadamu kutaka aachiliwe mara moja na apewe matibabu maalum. less

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3