Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TAHADHARI YATOLEWA NA TMA MVUA KUBWA LEO JUMAPILI MIKOA HII HAPA

TAHADHARI YATOLEWA NA TMA MVUA KUBWA LEO JUMAPILI MIKOA HII HAPA

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa angalizo la kuendelea kwa mvua kubwa kwa siku ya leo, Jumapili ya tarehe 15.03.2026, ikitarajiwa kuathiri maeneo machache katika mikoa tisa nchini.

Mikoa iliyoko kwenye hatari ya kukumbwa na hali hiyo ni pamoja na Ruvuma, Morogoro, Lindi, Mtwara, Mbeya, Iringa, Njombe, Dodoma, pamoja na Singida.

Kwa mujibu wa utabiri huo, uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa kiwango cha wastani, huku kukiwa na tahadhari ya athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo baadhi ya makazi kuzungukwa na maji kutokana na wingi wa mvua hizo.

Wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua hatua za tahadhari, kuzingatia ushauri wa kitaalamu, na kujiandaa na mabadiliko hayo ya hali ya hewa ili kuepuka madhara yanayoweza kuzitokea kwa binadamu na mali zao.



                 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3