Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MWANDISHI AMWANGUKIA DC KUHUSU MTOTO HUYO ,WAZIRI DKT GWAJIMA AOMBWA AINGILIE KATI

MWANDISHI AMWANGUKIA DC KUHUSU MTOTO HUYO ,WAZIRI DKT GWAJIMA AOMBWA AINGILIE KATI

Habari mheshimiwa  DC, pole na hongera kwa majukumu yako makubwa ya kuwatumikia wananchi.

Samahani kwa kukuandikia ujumbe huu, lakini tunaomba msaada wako kuhusu tukio la kusikitisha lililotokea katika Kijiji cha Kisirisiri, Kata ya Mjabibi, Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.

Kuna binti mwenye umri wa miaka 12 anayeitwa Neema ambaye ameozeshwa kwa nguvu na baba yake mzazi aitwaye Nashon Lucas. 

Binti huyo alifiwa na mama yake tangu akiwa mdogo sana, hivyo amekuwa akiishi chini ya uangalizi wa baba yake.

Mwaka juzi baba yake alijaribu pia kumuozesha dada yake Neema, lakini kwa bahati nzuri binti huyo alifanikiwa kutoroka na kwenda kuishi kwa bibi yake mzaa mama. Hata hivyo, baba huyo alifika hadi kwa bibi huyo na kumchomea nyumba.

Kwa bahati nzuri binti aliweza kuondoka katika kijiji hicho na hadi leo hajarejea tena.

Kwa sasa, taarifa tulizopata ni kwamba wiki iliyopita baba huyo amemuozesha binti huyo Neema kwa mwanaume ambaye tayari ana wake wawili, hivyo Neema amepelekwa kuwa mke wa tatu. 

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba binti huyo hajawahi kupelekwa shule kabisa.

Mheshimiwa DC, tunaomba msaada wako ili hatua za haraka zichukuliwe kumlinda mtoto huyu na kuhakikisha haki zake zinalindwa.

 Tunaamini msaada wako unaweza kuleta mabadiliko na kuokoa maisha ya mtoto huyu.

Mimi Zulfa Mfinanga,

Mwandishi wa Habari, nipo Arusha

Hata hivyo uongozi wa Matukio   Daima Media unaungana na mwandishi Zulfa Mfinanga kwa kumuomba Mkuu wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma pamoja na waziri wa maendeleo ya Jamii,Jinsia ,wanawake na makundi Maalum Dkt Doroth Gwajima kuingilia kati suala hili na Matukio Daima Media tunaimani kubwa na uwajibikaji wa mheshimiwa waziri pamoja na ujumbe huu kuupata kwa kuchelewa ila tunaamini ataufanyia kazi.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3