PROFESA KITILA MKUMBO ATAKA TISEZA KUCHOCHEA UWEKEZAJI WA VIWANDA KIGOMA
Na Fadhili Abdallah
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amezindua rasmi Kituo cha Huduma za Uwekezaji cha Kanda ya Magharibi cha Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) na kuhimiza shughuli za uwekezaji wa viwanda mkoani Kigoma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Mkumbo alisema kuwa kufunguliwa kwa Kituo hicho kunalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za uwekezaji pamoja na kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika Kanda ya Magharibi ili kuongeza fursa za ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuchangia kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Waziri huyo wa mipango na uwekezaji alisema kuwa kuwepo kwa Kituo hicho kutarahisisha upatikanaji wa huduma za uwekezaji pamoja na kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika Kanda ya Magharibi hasa wakati huu ambapo serikali imeuchagua mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati wa shughuli za uchumi na biasharaa kwa ajili ya soko la nchi za maziwa makuu.
Kituo hicho kinalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za uwekezaji pamoja na kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika Kanda ya Magharibi.
Amesema kuanzishwa kwa kituo hicho kutarahisisha upatikanaji wa taarifa, ushauri na huduma nyingine muhimu kwa wawekezaji, hatua inayotarajiwa kuchochea uanzishwaji na upanuzi wa shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali za Kanda ya Magharibi.
Aidha, Profesa Mkumbo ameeleza kuwa Mkoa wa Kigoma una umuhimu wa kimkakati katika kukuza biashara na uwekezaji kutokana na nafasi yake ya kijiografia inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Awali akizungmza katika uzinduzi huo Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalum ya kiuchumi Tanzania (TISEZA) , Gilead Teri alisema kuwa kufunguliwa kwa kituo hicho mkoani Kigoma kunalenga kusogeza karibu elimu na taarifa mbalimbali kuhusu taratibu za uwekezaji na namna wawekezaji wanavyoweza kufaidika na uwekezaji wao.
Teri alisema kuwa kwa sasa mamlaka hiyo iko tayari katika uelimishaji na kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji na kutoa witto kwa wawekezaji wa ndani na nje kuitumia ofisi hiyo kupata taarifa muhimu ambazo zitawasaidia kwenye mipango yao mbalimbali.
Mwisho.


