Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI ATARAJIWA LINDI KWA ZIARA YA SIKU TATU

MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI ATARAJIWA LINDI KWA ZIARA YA SIKU TATU

 


Na Hadija Omary, Lindi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi, anatarajia kufanya ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Lindi kuanzia Ijumaa tarehe 13 Novemba hadi Jumapili tarehe 15 Novemba 2026.

Akitoa taarifa ya ujio wa Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima, amesema katika ziara hiyo Makamu wa Rais atafanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Amesema miradi atakayokagua inahusisha sekta muhimu kwa wananchi ambazo ni afya, elimu, maji safi na salama, nishati, miundombinu ya barabara pamoja na kilimo.


Ameeleza kuwa katika ziara yake hiyo Ndejembi atatembelea Halmashauri ya Mtama, Lindi Manispaa na Kilwa ambapo katika maeneo hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais atapata fursa ya kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara, kusikiliza kero na changamoto zao, pamoja na kutoa mwelekeo wa Serikali na kuhamasisha shughuli za maendeleo na uchumi.


Hata hivyo, Malima ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo mgeni huyo atapita ili kumpokea kwa heshima na bashasha inayostahili.


Malima amesema kujitokeza kwa wingi ni ishara ya shukrani na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3