WAZIRI NYANSAHO ASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA AMANI NA USALAMA BARANI AFRIKA
Na Matukio Daima Media
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa.Dkt.Rhimo Nyansaho amesisitiza dhamira ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendeleza misingi ya umoja wa Afrika, usalama wa pamoja na ushirikiano wa kikanda.
Mhe.Waziri wameyasema hayo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa makamanda wa vyuo vya ukamanda na mafunzo ya kijeshi Barani Afrika.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi waandamizi wa kijeshi na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika , akiwemo Mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Mkuu wa Chuo cha ukamanda na Unadhimu Tanzania na Mwenyekiti wa mkutano wa makamanda wa vyuo vya kijeshi vya Afrika ( ACoC), Meja Jenerali Steven Justice Mkande, Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, wawakilishi wa umoja wa Afrika, Makamanda wa vyuo vya kijeshi , Wakufunzi wakuu na maafisa waandamizi wa kijeshi.
Mheshimiwa.Dkt.Rhimo Nyansaho aliwasilisha salam za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa washiriki wote wa mkutano huo
Mkutano huo umefanyika tarehe 11 Novemba 2026, Jijini Arusha
