Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WMA YAIMARISHA ULINZI WA WANANCHI DHIDI YA VIPIMO VISIVYO SAHIHI.

WMA YAIMARISHA ULINZI WA WANANCHI DHIDI YA VIPIMO VISIVYO SAHIHI.


NA CHAUSIKU SAID 
MATUKIO DAIMA MWANZA.

WAKALA wa Vipimo (WMA) imejipanga kuimarisha ulinzi wa wananchi dhidi ya matumizi ya vipimo visivyo sahihi kwa kuwafuata wafanyabiashara katika maeneo yao na kufanya uhakiki wa vifaa vinavyotumika katika shughuli mbalimbali.



Hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa ustahiki bila kuibowa na biashara kutokana na matumizi ya mizani na vipimo ambavyo havijahakikiwa na Wakala huo.



Akizungumza katika ufunguzi wa Maonesho ya 21 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya furahisha Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Vipimo (WMA), Christopher Mwakibinga, ameeleza kuwa wataendelea kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi.


Mwakibinga amesema kwa sasa WMA haitasubiri wananchi au wafanyabiashara kufika katika ofisi zake, bali itawafuata katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kutoa elimu na kufanya uhakiki wa vipimo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanatumia vifaa vya kupimia vilivyohakikiwa na Wakala wa Vipimo.


“Vipimo vilivyohakikiwa vinatambulika kwa urahisi kwa kuwa huwekwa alama maalumu pamoja na stika au stampu inayoonesha kuwa kifaa hicho kimekaguliwa,” Amasema Mwakibinga.


Mwakibimga amesema kuwa mbali na uhakiki wa vifaa vya kupimia, wanakagua bidhaa zilizofungashwa zinazozalishwa ndani ya nchi pamoja na bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi kupitia mipaka mbalimbali.


Aidha, ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaochezea au kulegeza mizani, akisema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kwamba Wakala huo umejipanga kuchukua hatua dhidi ya wahusika.


Hata hivyo, ameleza kuwa wataweka mkazo pia katika utoaji wa elimu, akibainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaweza kuwa wanakiuka sheria kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.


Kwa mujibu wa Mwakibinga, ameeleza kuwa wafanyabiashara wanaokiuka sheria kwa kutofahamu watapatiwa elimu, lakini wale watakaobainika kufanya ukiukwaji huo kwa makusudi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3