Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
*WAZIRI MAVUNDE AONGOZA KIKAO CHA UTATUZI MGOGORO WA HAKI MADINI NA HAKI ARDHI*

*WAZIRI MAVUNDE AONGOZA KIKAO CHA UTATUZI MGOGORO WA HAKI MADINI NA HAKI ARDHI*


*Dodoma*

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, akiongoza kikao cha utatuzi wa mgogoro wa haki madini na haki ardhi baina ya Kampuni ya Barrick na wachimbaji wadogo wa madini wa Tarime,Mkoani Mara.

Kikao hicho cha maridhiano, kimefanyika  leo tarehe 4 Septemba, 2026, jijini Dodoma ambapo Waziri Mavunde amezitaka pande zote mbili  kukaa na kujadiliana ili kuangalia namna ya bora ya kufika muafaka kwa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Madini Sura 123.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na  Mkuu wa Wilaya Tarime, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, Wawakilishi wa mgodi wa North Mara na walalamikaji.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3