WENGER: SIKUHUSISHWA KWENYE MPANGO WA KUUZA HISA ZA FIFA
Aug 4, 2026
Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Arsène Wenger amethibitisha kuwa hakuwa ameshirikishwa kwenye mchakato wa Rais Gianni Infantino wa kutaka kuuza hisa za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).
Kulingana na Wenger, ambaye kwa sasa anahudumu kama Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka ndani ya FIFA, amesikia madai ya kutaka kuuzwa kwa hisa katika haki za kibiashara za Kombe la Dunia, kupitia vyombo vya habari pekee.
Hata hivyo, mpango huo umekwama, baada ya kupata upinzani mkali kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka duniani.
