Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
AJALI MBAYA ZASABABISHA VIFO MORO, LIMO BASI LA ABIRIA NA LORI LA MBAO YALIYOGONGANA NA KUWAKA MOTO, KWINGINE NI GARI YA POLISI

AJALI MBAYA ZASABABISHA VIFO MORO, LIMO BASI LA ABIRIA NA LORI LA MBAO YALIYOGONGANA NA KUWAKA MOTO, KWINGINE NI GARI YA POLISI



Na Matukio Daima Media, Morogoro

MOROGORO: Watu kadhaa ambao idadi yao haijafahamika mara moja wanahofiwa kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mbao na kisha magari hayo kuteketea kwa moto katika eneo la Mkambalani, Wilaya ya Morogoro, mkoani Morogoro.

Ajali hiyo imetokea katika barabara kuu ya Morogoro–Dar es Salaam, huku taarifa za awali zikieleza kuwa baadhi ya watu waliokuwa kwenye magari hayo wamefariki na wengine huenda wamejeruhiwa.

Katika tukio jingine, ajali imeripotiwa kutokea usiku katika eneo la Mkambarani, Dakawa, kwenye barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, ambapo basi na lori vinadaiwa kugongana na kuteketea kwa moto.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali hizo, huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Aidha, katika eneo jingine ndani ya Halmashauri ya Morogoro, watu wamehusishwa na ajali inayodaiwa kuhusisha gari la Polisi na gari jingine, ingawa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo bado hayajafahamika.

Matukio Daima Media inaendelea kufuatilia taarifa hizi na itatoa idadi rasmi ya waliopoteza maisha na waliojeruhiwa mara baada ya kupata uthibitisho kutoka kwa mamlaka husika.

FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2027 MEDALA HIGH SCHOOL IDODI IRINGA

 

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 0753549368 AU 0736313160

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3