ALIYEKUWA KATIBU CCM MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI
Oct 11, 2026
Taarifa iliyotufikia hivi punde ni kuwa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Said Goha amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mbezi Luis jijini Dar es salaam kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa James Mgego amethibitisha alipoulizwa na Matukio Daima Media kwa njia ya simu ,Goha alikuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa na wiki mbili sasa zimepita toka Katibu wa itikadi Paul Chacha alipomtamgaza kwenye mkutano mkuu maalum wa CCM mkoa wa Iringa uliofanyika chuo cha UVCCM Ihemi kuwa amemsimamisha kazi kwa madai ya ulevi na kumtaka kuripoti makao makuu ya CCM kwa majukumu mengine na nafasi yake siku chache kukaimiwa na James Mgego ambae anakaimu hadi sasa.siku Goha (Kushoto) alivyokabidhi ofisi kwa kaimu katibu wa Mkoa wa Iringa James Mgego
Goha akitoa neno la mwisho akiwaaga watumishi ofisi ya CCM mkoa wa Iringa
Goha akizungumza na MCC Salim Asas















