Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NDUGU WA MTOTO HUYU WANATAFUTWA ,ALINUSURIKA AJALI ILIYOUA MAMA NA KAKA YAKE..

NDUGU WA MTOTO HUYU WANATAFUTWA ,ALINUSURIKA AJALI ILIYOUA MAMA NA KAKA YAKE..

 


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga inawatafuta ndugu au jamaa wa mtoto huyu wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5, ambaye hajafahamika jina lake. 


Mtoto huyo alinusurika katika ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 20 Juni 2026 eneo la Wendele, iliyohusisha gari la kampuni ya OG Classic lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Geita. Katika ajali hiyo, mama yake, kaka yake na watu wengine wanne walipoteza maisha. Kwa sasa mtoto anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu. 


Iwapo unamfahamu au una taarifa zinazoweza kusaidia kumpata ndugu au jamaa zake, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Ustawi wa Jamii kupitia namba: 0782 495 133


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3