Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MIMI SIO MAKAMU WA RAIS WA CCM,NI WA VYAMA VYOTE - NDEJEMBI

MIMI SIO MAKAMU WA RAIS WA CCM,NI WA VYAMA VYOTE - NDEJEMBI



NA MATUKIO DAIMA MEDIA

DODOMA. Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa kura zote 304 sawa na asilimia 100, atakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wote bila kujali vyama vyao vya siasa.

Ndejembi amesema hayo leo Agosti 28, 2026, muda mfupi baada ya kuthibitishwa na Wabunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema atatekeleza majukumu yake kwa unyenyekevu na kuhakikisha anakuwa kiungo kati ya Serikali na Watanzania wote, huku akisisitiza kuwa atafanya kazi kwa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ninakuwa ni Makamu wa Rais wa Watanzania wote, nakuwa Makamu wa Rais si wa wana CCM peke yake, nakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wa vyama vyote.”

Amesema atatumia nafasi hiyo kwa unyenyekevu mkubwa katika kumsaidia Rais na kuwa kiungo cha Watanzania wote.

“Nitajitahidi kwa unyenyekevu mkubwa sana kumsaidia Mheshimiwa Rais, kuwa kiungo wa Watanzania wote kama vile mapenzi yake yatakavyotaka, kwa sababu nafanya kazi chini yake.”amesema

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3