Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
COPRA YAHAMASISHA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA KUTUMIA MIFUMO BUNIFU YA KIDIGITALI

COPRA YAHAMASISHA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA KUTUMIA MIFUMO BUNIFU YA KIDIGITALI


Na Lilian Kasenene, Morogoro

Matukio DaimaApp 

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (COPRA) imeendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao mbalimbali kuhusu matumizi ya mifumo bunifu ya kidigitali ili kuboresha biashara ya mazao nchini.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa COPRA, Merry Majule, wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro.


Majule alisema mamlaka hiyo inawahamasisha wakulima na wafanyabiashara kujitokeza katika banda la COPRA ili kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya biashara ya mazao, ikiwemo usajili, uuzaji wa mazao ndani na nje ya nchi pamoja na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili kuhakikisha biashara inafanyika kwa haki na ushindani.


"Katika banda letu pia tunatoa darasa kwa wadau mbalimbali na wakulima kuhusu mifumo yetu ya kidigitali na namna wanavyoweza kuitumia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na COPRA," alisema.


Alieleza kuwa COPRA inatekeleza majukumu yake kupitia nguzo mbalimbali ambazo ni uimarishaji wa uzalishaji na biashara ya mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko, uboreshaji wa mifumo bunifu ya kidigitali na takwimu, kuimarisha masoko yenye ushindani na yanayoratibiwa, kuimarisha utendaji wa taasisi pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa sekta hiyo.


Aidha, alisema COPRA imeanzisha mfumo wa kidigitali wa **COPRA MIS**, unaowezesha utoaji wa leseni na vibali, usimamizi wa mikataba ya kilimo kati ya wakulima na wanunuzi au wawekezaji, pamoja na uhakiki na ufuatiliaji wa ubora wa mazao kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.


Aliongeza kuwa mfumo huo pia unasaidia kufuatilia mazao katika mnyororo mzima wa thamani kuanzia shambani hadi sokoni, hatua inayochangia kuongeza uwazi, ufanisi na ushindani katika biashara ya mazao.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3