ASKOFU DKT MPELI AMPA POLE MKURUGENZI MATUKIO DAIMA KWA KIFO CHA KAKA YAKE
Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, uwepo wako, maneno yako ya faraja, maombi na ushirika wa kiroho vimekuwa chanzo kikubwa cha nguvu, tumaini na faraja kwa familia nzima.
Umeonyesha kwa vitendo kuwa mchungaji wa kweli anayesimama na waumini na jamii katika nyakati za furaha na huzuni.
Tunamshukuru Mungu kwa kukujalia hekima, moyo wa upendo na utumishi wenye kugusa maisha ya watu wengi.
Tunatambua kuwa huduma yako ya kuwafariji wenye huzuni ni sehemu ya wito wa Mungu wa kuponya mioyo iliyovunjika na kuwatia watu nguvu ya kuendelea mbele kwa imani.
Neno la Mungu linasema katika 2 Wakorintho 1:3–4: “Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote; atufarijie katika dhiki zetu zote, ili na sisi tupate kuwafariji walio katika dhiki yo yote, kwa faraja ile ile ambayo sisi wenyewe tunafarijiwa na Mungu.”
Kwa niaba ya Francis Godwin, familia yake na timu nzima ya Matukio Daima Media, tunasema asante sana kwa upendo wako wa dhati, maombi na faraja yako. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda, akupe afya njema, akuongezee neema na kuibariki huduma yako ili uendelee kuwa chombo cha amani, tumaini na baraka kwa watu wengi.
Mungu akubariki sana, Askofu Dkt. Mpeli James Mwaisumbe.
