Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
ARSENAL YAKAMILISHA DILI LA BRUNO GUIMARES KWA PAUNI MILIONI 75

ARSENAL YAKAMILISHA DILI LA BRUNO GUIMARES KWA PAUNI MILIONI 75


Arsenal imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo Bruno Guimarães kutoka Newcastle United kwa ada inayokadiriwa kufikia £75 milioni. Taarifa zinaeleza kuwa pande zote zimekubaliana, huku vipimo vya afya vikitarajiwa kufanyika ndani ya wiki hii kabla ya mchezaji kusaini mkataba wa muda mrefu.

Bruno amekuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa kwenye orodha ya kipaumbele ya Mikel Arteta kwa muda mrefu, na sasa usajili huo unaelekea kukamilika ikiwa hatua za mwisho zitapita kama zilivyopangwa.

Unauonaje usajili huu? Je, Bruno Guimarães ndiye kiungo ambaye Arsenal imekuwa ikimhitaji ili kupigania ubingwa?

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3