YERICKO NYERERE KUICHANGIA CHAUMMA TSH MILIONI 12
IRINGA.
Siku moja baada ya Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma ((CHAUMMA), Benson Kigaila kuzindua operesheni mpya ya chama hicho ya "Tujenge Pamoja#Tanzania ni Sisi" ikamilike, Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanaharakati wa Tanzania Yeriko Nyerere amesema atakuwa akichangia chama kicho kiasi cha shilingi million moja kila mwezi.
Yericko ametoa kauli hiyo leo wakati akifanya mahojiano na Matukio Daima Media katika kipindi cha asubuhi ya moto kwa njia ya siku na kubainisha kuwa uendeshaji wa chama cha siasa cha CHAUMMA unategemea michango ya wanachama wake badala ya kutegemea wafadhili.
Aidha alisistiza kuwa kuwa ushiriki wa kila mwanachama ni msingi wa kukijenga na kukiimarisha chama na kuwataka wanachama wengine wenye uwezo kuiga mfano huo ili kukiwezesha chama kutekeleza shughuli zake za kisiasa na maendeleo.
“Mimi binafsi nimejitolea kuchangia shilingi milioni moja kila mwezi, sawa na shilingi milioni kumi na mbili kwa mwaka, katika operesheni ya kuchangia CHAUMMA”alisema
Aidha, alieleza kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhamasisha michango hiyo kwa uwazi kupitia mitandao ya kijamii, akiwataka wananchi kushiriki katika kujenga chama chao na kuhakikisha michango yote inafanyika kwa uwazi na kutolewa risiti kwa kila mchangiaji.
