Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MGONANZI ATAKA WAZAZI KUSIMAMIA MALEZI BORA YA WATOTO KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA

MGONANZI ATAKA WAZAZI KUSIMAMIA MALEZI BORA YA WATOTO KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA: 

Mdau wa masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia, Yohana  Ng’eng'ena  maarufu kama Mgonanzi  amewataka wazazi kurejea katika misingi bora ya malezi ili kupunguza vitendo vya ukatili vinavyoendelea kujitokeza katika familia na jamii.


Akizungumza na matukio daima Mgonanzi amesema familia ndiyo msingi wa kumjenga mtoto na kwamba wazazi hawawezi kuhamishia jukumu lote la malezi kwa shule au walimu. Amesema watoto wanahitaji uangalizi wa karibu na mazungumzo ya mara kwa mara ili kuwajenga katika maadili mema.


Ameeleza kuwa kutokana na wazazi wengi kuwa bize na shughuli za kutafuta kipato, watoto wengi hubaki bila uangalizi nyumbani, hali inayowaweka katika mazingira ya kuathiriwa na tabia zisizofaa au kufanyiwa ukatili.

“Mtoto hupitia hatua mbalimbali za ukuaji na hukutana na mazingira tofauti kuanzia chekechea hadi chuo, hivyo ni muhimu wazazi kuweka msingi imara wa maadili mapema ili aweze kufanya maamuzi sahihi anapokutana na changamoto”alisema


Aidha Mgonanzi amesisitiza kuwa wazazi wanapaswa kuwafuatilia watoto wao, kufahamu marafiki zao, kusikiliza changamoto zao na kuwapa muda wa kutosha, badala ya kuamini kuwa jukumu hilo linaweza kutekelezwa na taasisi nyingine pekee.


“Nawahimiza wazazi wanaolea watoto peke yao kutokata tamaa, kwa kuwa mtoto anahitaji zaidi upendo, mwongozo na maadili mazuri kuliko mazingira ya kifedha pekee ili kukua akiwa raia mwema

“.

Mgonanzi pia ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika kuimarisha malezi ya watoto, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza ukatili wa kijinsia na kujenga kizazi chenye maadili, uwajibikaji na heshima kwa wengine.

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3