Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RAIS SAMIA AIPONGEZA TWIGA STARS

RAIS SAMIA AIPONGEZA TWIGA STARS

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco kwa ushindi wa bao 2 -1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, (Banyana Banyana).

"Ninaipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars), kwa kuanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco kwa ushindi dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, (Banyana Banyana).Ninaungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri Twiga Stars inapoendelea kupeperusha bendera ya Taifa letu katika michezo inayofuata. Endeleeni kupambana kwa moyo huo huo, mkionesha uzalendo, nidhamu na ari ya ushindani inayolitangaza vyema Taifa letu".Ameandika Rais Samia katika ukurasa wake wa Instagram


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3