CDF MKUNDA ATOA AGIZO KWA ASKARI JWT
Jul 22, 2026
Na Matukio Daima Media
Mkuu wa Majeshi (CDF) Jenerali Jacob Mkunda amewaagiza maofisa na Askari wa Jeshi la Wananchi la Tanzania kuendelea kujituma ikiwamo kuzidisha nidhamu ndani na nie ya kazi ili kuimarisha amani nchini.
Kadhalika amesema michezo si mashindano bali pia ni burudani inayoimarisha mshikamano wa Kamandi zote za JWTZ.
CDF Mkunda alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mashindano ya CDF CUP 2026.
Awali Kamandi sita zilizoshiriki mashindano hayo zilikabidhiwa vikombe na tuzo za michezo mbalimbali.

