Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WATUMISHI 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, 9 SHAURI LAO LINAENDELEA

WATUMISHI 12 WAFIKISHWA MAHAKAMANI, 9 SHAURI LAO LINAENDELEA

 


Na Matukio DaimaMedia 


Watumishi 12 wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni na Ofisi ya Rais Tamisemi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za wizi na ubadhilifu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 169,617,520 maarufu kama (FEDHA ZA BAKAA)


Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 2,2026 jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke Francis Luena wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha  Mwezi Januari hadi Machi,2026.


Luena amesema kuwa uchunguzi ulifanyika kwa mujibu wa sheria na mwezi Septemba 2,2025 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa ya kuendesha genge la uhalifu,uchepuzi, ubadhilifu,utakatishaji fedha na kuisababishia hasara Serikali,makosa ambayo ni kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi Na.200,sheria ya kuzuia na Kupambana na rushwa Na.329, na sheria ya utakatishaji fedha Na.423.


"Waliofikishwa mahakamani ambao ni watumishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na vyeo vyao kwenye mabano ni Annie Nyabugumba(Afisa Hesabu Mwandamizi),Tumsifu Christopher Kachira(Afisa Hesabu Mwandamizi daraja la I ), na Aidan Zabron Mponzi( Afisa Hesabu daraja la l ) "amesema Luena 


Nakuongeza kuwa"Watumishi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni Jonathan Stanley Manguli(alikua Mkuu wa kitengo Cha MUSE),Godfrey James Martiny(Muweka Hazina),Juvenalis Babilas Mauna(Mkuu wa kitengo cha kudhibiti taka na usafi wa Mazingira),Josephat Mutembei( mhandisi),Bibiana Romanus Mdete( mtunza Bohari) na Henry Herman Rugayi(Afisa ugavi).


Wengine watatu ni wafanyabiashara ambao ni Hamis Kashinje Manfred,(Mkurugenzi Mtendaji Konya Investment Co.LTD),Paul Sam Mwakyusa(mmiliki wa mbogholo Investment Co.LTD),Godwin Adamson Cheyo( mmiliki wa Macheye Tz Investment).


Hata hivyo amefafanua kuwa kufikia Machi 2026 washtakiwa watatu Juvenalis Babilas Mauna,Josephat Mutembei na Hamis Kashinje Manfred walikiri makosa yao kupitia makubaliano (plea bargain) na wamerejesha jumla ya kiasi cha shilingi milioni 87,na kulipa faini ya shilingi Milioni 3.5


"Mshtakiwa Juvenalis Babilas Mauna amerejesha shilingi milioni 27,nakulipa faini ya shilingi milioni 2,Hamis Kashinje Manfred amerejesha shilingi milioni 40,na kulipa faini ya shilingi milioni 1.5,na Josephat Mutembei amerejesha shilingi milioni 20,huku washtakiwa 9 waliobakia Shauri lao linaendelea mahakamani."Amesema.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3