TETEMEKO KUBWA UFILIPINO LAUA 37, MAELFU WAKIMBIA MAKAZI
Jun 9, 2026
Zaidi ya watu 20,000 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia tetemeko kubwa lililotokea kusini mwa Ufilipino, ambalo pia limesababisha vifo vya watu 37.
Mamlaka za usimamizi wa maafa nchini humo zimesema kuwa uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu umewalazimu wakazi wengi kuhama maeneo yao na kutafuta hifadhi salama.
Waokoaji wanaendelea kufanya kazi ya kutafuta watu ambao huwenda wamenaswa chini ya vifusi vya majengo yaliyobomoka, huku juhudi za misaada ya kibinadamu zikiendelea kuwafikia waathirika.
Serikali ya Ufilipino imesema inaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu na kuhakikisha msaada unawafikia wote walioathirika na janga hilo.