Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
GACHAGUA KULIPWA FIDIA KSH MILION 50 SAWA NA BILION 1 YA KITANZANIA

GACHAGUA KULIPWA FIDIA KSH MILION 50 SAWA NA BILION 1 YA KITANZANIA


Mahakama Kuu ya Kenya imeidhinisha rasmi mchakato wa kung’olewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua huku ikiamuru alipwe fidia ya Ksh. mil 50 (sawa na bilioni 1 za Kitanzania) kama suluhu ya ukiukwaji wa haki zake wakati wa mchakato wa kuondolewa madarakani.

Uamuzi huo umetolewa Juni 8, 2026 na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Eric Ogola ambao walianza kusoma hukumu hiyo kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 3:00 usiku kutokana na ukubwa wa nyaraka za kesi hiyo.

Katika uamuzi wao, Majaji wamesema kuwa mchakato uliofanywa na Bunge la Taifa na Seneti ya Kenya ulifuata taratibu zote za Kikatiba na pia hawakupata ushahidi wa kuonyesha kuwa haki ya Gachagua ya kusikilizwa ilikiukwa.

Pia Mahakama imeamuru Bunge la Kitaifa na Seneti kumlipa fidia hiyo kutokana na kukiukwa kwa haki za Gachagua wakati wa shughuli za Seneti.

Gachagua alikuwa akihoji uhalali wa uamuzi wa Bunge na Seneti ya mwaka 2024 uliosababisha kuondolewa kwake madarakani kwa tuhuma mbalimbali, zikiwemo ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa uamuzi huu wa Mahakama Kuu, hoja zake zote za kupinga ‘impeachment’ zimetupiliwa mbali na mchakato wa kumuondoa madarakani umeendelea kubaki halali kikatiba.

Itakumbukwa kwamba Gachagua alikuwa Naibu Rais katika Serikali ya Rais William Ruto.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3