Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KUWASA YAPANDISHA GHARAMA BILI ZA MAJI KIGOMA UJIJI

KUWASA YAPANDISHA GHARAMA BILI ZA MAJI KIGOMA UJIJI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) imefanya mabadiliko ya gharama ya bili za maji kwa wateja wake kwa shilingi 500 kwa wateja wa majumbani huku ikielezwa kuwa gharama za uendeshaji ndiyo zilizochangia kuwepo kwa ongezeko hilo.

Akitangaza mabadiliko hayo ya bei Afisa mipango na uchumi wa KUWASA, Naaman Kahoye kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Dk.Christopher Nditi alisema kuwa bei za huduma ya maji kwa wateja wa majumbani zimepanda kutoka shilingi 1415 kwa Unit moja za awali na bei mpya kufikia 1850 zitaanza kutumika rasmi Julai Mosi mwaka huu.

Kahoye alisema kuwa kwa wateja wa Taasisi gharama imepanda kutoka shilingi 1700 inayotumika kwa sasa na kufikia shilingi 2253, wateja wa biashara na viwanda bei imepanda kutoka shilingi  1800 na kufikia shilingi 2385.

Akizungumza katika mkutano huo wa kutangaza bei mpya Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA,Dk.Chiristopher Nditi alisema kuwa mamlaka hiyo imekumbwa na changamoto kubwa kutokana na mapato kutokidhi hali halisi ya uendeshaji jambo linalowafanya kuongeza bei ya maji ili kuendesha na hali halisi ya uendeshaji,

Katika hilo alisema kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto ya mivujo mikubwa ya maji kutokana na miundo mbinu chakavu hivyo mpango wa mamlaka ni kubadilisha na kuboresha miundo mbinu, Kupunguza madeni kwa taasisi za serikali kwa kufunga Prepaid water meters kwa wateja 300 na mita 18,000 kwa  majumbani na  Kuongeza mtandao wa maji katika maeneo yenye uhitaji kwa umbali wa kilometa 200.


Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3