KIPAJI CHA TANZANIA CHATUA FC BARCELONA
Jun 9, 2026
Kinda wa Kitanzania Barka Seif Mpanda ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kusajiliwa katika Akademi ya Klabu ya Barcelona La Marsia akitokea katika akademi ya CF Damm ya nchini Uhispania.
Usajili huo unakuja baada ya kuonyesha kiwango bora sana akifunga magoli 41 katika michezo 28 tu Hali iliyovutia uingozi wa La Marsia na kuamua kumsajili
“Ndoto zangu zimetimia kujiunga na La Marsia, naushukuru uongozi wa CF Damm kwa kunisaidia katika misimu mitatu niliyokuwa nao, nawashukuru makocha, wachezaji wenzangu na familia kwa kufanikisha jambo hili”
