Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MEXICO YAAHIDI UFUNGUZI BORA KOMBE LA DUNIA

MEXICO YAAHIDI UFUNGUZI BORA KOMBE LA DUNIA

 

Rais Claudia Sheinbaum wa Mexico ametoa hakikisho la kuwepo utulivu wakati wa mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia baadae wiki hii, licha ya wasiwasi kutokana na maandamano yanayoendelea.

Muungano wa walimu nchini humo umetishia kufanya maandamano makubwa kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Mexico na Afrika Kusini itakayofanyika kwenye mji mkuu, Mexico City ikiwa serikali haitotimiza madai yao ya nyongeza za mishahara na pensheni. 

Kwenye mkutano wake wa kila siku na waandishi habari, Bibi Sheinbaum amesema serikali yake itahakikisha sherehe za Kombe la Dunia zinafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. 

Wiki iliyopita, polisi iliwatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi na risasi za mpira nje ya uwanja mkubwa wa Zocalo ambao umetengwa kwa mashabiki wasiokwenda uwanjani, kutizama mechi kupitia televisheni.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3