ALIYEMUUA MWALIMU HERIETH AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
Na Matukio Daima Media, Mbeya
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa Barnaba Daud Mtewele mkazi wa Wilayya ya Chunya Mkoani Mbeya baada ya kummtia hatiani kwa mauaji ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Herieth Lupembe(37),Ivon Tatizo mwanafunzi wa kidato cha pilli Isenyela na kumjeruhi Daud Barnaba Mtewele(7) machi 31,2023.
Katika kesi hiyo Jamhuri imewakilishwa na Wakilii Augustino Magesa na mshitakiwa Barnaba Mtewele amewakilishwa na Wakili wa kujitegemea Joyce Kasebwa.
Akitoa hukumu iliyodumu kwa saa mbili kuanzia saa 9:30 alasili hadi saa 11:30 jioni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mheshimiwa Joackim Charles Tiganga amemtia hatiani Barnaba Daud Mtewele kwa makosa matatu mawili ya mauaji ya Mwalimu Herieth Lupembe na Ivon Tatizo pia kujeruhi Daud Barnaba Mtewele ambaye alilazwwa hospitali ya Wilaya ya Chunya,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Benjamin Mkapa.
Akisoma hukumu Jaji Tiganga amesema upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi nane pamoja vielelezo mbalimbali na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wanne na kielelezo kimoja.
Ilielezwa Mahakamani kuwa Barnaba Mtewele alizaa na Mwalimu Heriety Lupembe mtoto Daud Barnaba(7)alliyetoa ushahidi wake mbaye aliileza mahakama kuwa mara kadhaa baba yake alikuwa akija mara wa mara na kula pamoja na wakati mwingine kuingia chumbani na siku ya tukio anachokumbuka baba yake alimpiga mama yake na dada yake kwa sululu kisha naye alipigwa na sululu.
Aidha shahidi baada ya kupigwa na sululu alipoteza fahamu na kuvuja damu nyingi ambapo baada ya siku kadhaa alipata fahamu ndipo alipoeleza kuwa muhusika wa matukio yote ni baba yake mzazi licha ya kuulizwa na Waakili wa utetezi bado ushahidi kutingisha.
Shahidi mwingine ni ndugu wa Herieth aliyeiambia mahaakama kuwa Daud akiwa hospitali alimwammbiia kuwa baba yake ndiye aliyempiga na sululu mama yake,dada yake na yeye .
Katika ushahidi mwingine ni daktari aliyeifanyia uchunguzi miili ya marehemu Herieth nna Ivon ambaye aliimbia mahakama kuwa vifo vimesabaabiisha na mvujo wa damu nyingi.
Pia Askari wa Upelelezi Wilaya alitoa ushahidi ambapo alisema alipokea taarifa kuttoka kwa balozi baada ya kumtafuta kwa simu na kwenda kwake milango yote ilikuwa imefungwa kwa nje ndipo walipovunja walikuta miili ina majeraha na damu ikkiwa imetapakaa na Polisi wallipofika walikuta eneo la tukio kuna sululu na miili miwili ilithibitishwa kuwa ni ya Herieth, Ivon na mtoto Daud ambaye alikuwa amepoteza fahamu.
Ushahidi mwingine uliotolewa ni pamoja Daktari aliyemtibu Daud Barnaba aliyedai kuwa Daud alijeruhiwa katika fuvu la kichwa na kuvuja damu nyiingi halii iliyosababisha kupoteza fahamu.
Mhemiwwa Jaji Joackim Tiganga amesema kifungu cha 117 na 118(iiii)(a) sura ya 6 iliyofanyiwa marejeo 2023 inautaka upande wa mashitaka kuthibitisha pasipo shaka kwa kuona au ushahidi wa kimazingira pia kuzingatia kifungu cha 211(i)((ii),211(a) na 380(i) sura yya 16 iliyoffanyiwa marejeo mwaka 2003 ambayo inaamtia hatiani mtu yeyote mweenyye nia ya kutenda kosa,kupanga hata kama kiitendo hicho hakkijafikia mwisho.
Upande wa utetezi mshitakiwa alileta mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni cheti cha ubatizo kwani mshiitakiwa alidai siku ya tukio hakwenda nyumbaani kwa Herieth badala yake alikuwa ibadani Kanisa la Angliikana Chunya alikosimamia ubatizo na yeye kurejea nyumbani ingawa ushahidi wake haukuthibitishwa na mkewe kuwa siiku hiyo alirejea nyumbani au la.
Pia ushahidi wa Katekista Mapunda,Joyce ,Kayombo hauthibitishi kuuwa baada ya ibada mshiitakiwa alikuwa wapi licha ya kuwasilisha cheti cha ubatizo bado hakioneshi kusajiliwa katika kitabu cha kanisa.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili Wakili wa serikali Augustino Magesa aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwa mujibu wa sheria ambapo wakili wa utetezi aliomba mahakama kuona namna ya kutoa adhabu kwa mtuhumiwa ni kosa lake lla kwanza.
Jaji alihitiimisha shauri hilo kwa kumhukumu Barnaba Mtewele kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua Herieth Lupembe na Ivon Tatizo pia kifungo cha miaka kumi kwa kumjerihii Daud Barnaba.
Rufaa iko wazi kwa upande ambao haujaridhishwa na uamuzi uliotolewa.
