Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WATU 118 WAFARIKI KUTOKANA NA EBOLA NCHINI DRC

WATU 118 WAFARIKI KUTOKANA NA EBOLA NCHINI DRC

 

Picha ya mhudumu wa afya akimulekekeza mgonjwa kunawa mikono

Takriban vifo vya watu 118 vimeripotiwa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini DRC, huku Zaidi ya maambukizi 390 yakiripotiwa, kulingana na shirika la kudhibiti magonjwa afrika (Africa CDC)

Mkurugenzi wa CDC barani Afrika, Jean Kaseya ameonya kuwa hakuna dawa ya kutibu aina hii ya Ebola, na umakini unafaa kuzingatiwa pakubwa na wahudumu wa afya na wakati wa mazishi ya walioathirika na ugonjwa huu.

Visa viwili vya ugonjwa huu vimeripotiwa nchini Uganda, na kisa kimoja cha kifo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa janga la kimataifa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3