WAISLAMU KOTE DUNIANI WANAADHIMISHA SHEREHE ZA EID AL-ADHA
May 26, 2026
Waislam kote duniani wanasherehekea sherehe za Idd al-Adha, zinazofanyika wakati wa Hija inayofanyika kila mwaka mjini Mecca.
Sherehe hiyo ambayo pia hufahamika kama sherehe ya kutoa kafara, ni moja kati ya sherehe kubwa za kiislam.
Ni kumbu kumbu ya kujitolea kwa utashi kwa Abraham kumtoa kafara mwanae kwa Mungu na wakati wa sherehe hii waislam hutoa kafara wanyama.
Wanawake wakihudhuria ibada katika jimbo la Bandeh Aceh, Indonesia
Katika soko la wanyama la Ashmun cattle nchini Misri, wafanyabiashara wakiuza wanyama kwa ajili ya kafara kabla ya sherehe za Eid al Adha