Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SHEKHE KIBURWA ATAKA DINI, SIASA ZIWAUNGANISHE WATANZANIA

SHEKHE KIBURWA ATAKA DINI, SIASA ZIWAUNGANISHE WATANZANIA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SHEKHE wa mkoa Kigoma Hassan Iddi Kiburwa amewaongoza viongozi na waumin wa dini ya kiislam katika sala ya Eid El Haji iliyofanyika Kimkoa Mjini Kigoma huku akiwataka Watanzania kutumia dini zao na itikadi zao za vyama vya siasa kiwaunganisha watanzania badala ya mambo hayo kuwatenganisha na kuwa maadui.

Katika sala hiyo iliyofanyika  kwenye uwanja wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma Shekhe huyo wa  kimkoa alisema kuwa dini zote zinafundisha waumini wake kuwa wanyenyekevu kwa Muumba wao na kupendana wao kwa wao hata kama mtu siyo wa dini yako lakini lazima upende na Amani uwepo baina ya wanadamu.

Shekhe Kiburwa alisema kuwa suala la upendo na Amani haliishi kwenye misingi ya dini lakini linapaswa kuwa kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu na kutaka chuki kna uhasama uliopo baina ya Watanzania kutokana na mitazamo tofauti ya vyama vya siasa haipaswi kuwagawa watanzania na kuharibu nchi zao.

Alisema kuwa matukio ya Oktoba 29 tayari yameanza kufanyiwa kazi na seerikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshaanza kuchukua hatua kukabili hilo na kwamba baada ya hatua mbalimbali serikali imekusudia kuwepo kwa maridhiano baina ya pande zote ili kuwarudisha Watanzania kuwa kitu kimoja kwa ajiili ya maslahi ya nchi yao.

Kwa upande wake Kadhi Mkuu wa Istiqama Foundation, Mustapha Kiumbe alisema kuwa wanadamu wanapaswa kubebeana madhaifu yao na kusameheana pale ambapo mmoja anakosea na kwamba chuki zinazotokana na matukio ya Oktoba 29 hazipaswi kuharibu nchi na kuiingizza kwenye migogoro.

Viongozi na waumini wa Msikiti wa Alhuda uliopo Nazareth Manispaa ya Kigoma Uijij wakishiriki katika zoezi la kuchinija ambapo ng'ombe wanne walichinjwa na kugawiwa kwa waumin mbalimbali.

Akizungumzia ibada ya kuchinja Shekhe Kiumbe aliwataka waislam kuhakikisha wanafanya kichonjo kitakatifu kwa kuchinja wanyama waliokomaana walionona na kugawa kwa watu mbalimbali ili kukamilisha ibada ya Eid huku akihimiza waislam nchini kuchinja wanyama wao wenyewe badala kusubiri misaada ya nyama kutoka nje.


Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3