Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NSOMBA ASISITIZA UMOJA CCM, AONYA WANAOANZA KAMPENI KABLA YA MUDA.

NSOMBA ASISITIZA UMOJA CCM, AONYA WANAOANZA KAMPENI KABLA YA MUDA.


 Samwel Mpogole - Mbeya.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Afrey Nsomba, amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuimarisha umoja, upendo na mshikamano huku akionya dhidi ya tabia ya kuanza kampeni mapema kuelekea uchaguzi wa ndani ya chama unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Katika mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha chama ngazi za matawi na kata, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Afrey Nsomba, ametembelea Kata ya Nzovwe ambapo amekutana na wanachama na viongozi wa chama hicho.

Akizungumza katika ziara hiyo, Nsomba amesisitiza umuhimu wa wanachama kushikamana na kudumisha umoja na upendo, akieleza kuwa mafanikio ya CCM yanategemea mshikamano wa wanachama wake.

Aidha, amewataka wanachama kuepuka vitendo vya kuanzisha kampeni kabla ya muda rasmi kuelekea uchaguzi wa ndani ya chama unaotarajiwa kufanyika mwakani, akisisitiza kuwa kila mwanachama anapaswa kuheshimu taratibu, kanuni na miongozo ya chama.

Nsomba amesema viongozi na wanachama wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kuijenga CCM na kutatua changamoto za wananchi badala ya kujihusisha na makundi yanayoweza kuhatarisha umoja wa chama.

Ziara hiyo ni sehemu ya mpango wa uongozi wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini wa kuendelea kukutana na wanachama katika kata mbalimbali kwa lengo la kusikiliza maoni yao na kuimarisha mshikamano ndani ya chama.




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3