Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NONDO AOMBA DIRISHA LA PILI LA MIKOPO LIFUNGULIWE

NONDO AOMBA DIRISHA LA PILI LA MIKOPO LIFUNGULIWE

 



Na Matukio DaimaApp 


Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa Chama ACT Wazalendo, Abdul Nondo ametoa wito kwa Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Vijana kufungua dirsha jipya la mikopo ili kutoa fursa kwa kundi lingine kuomba mikopo hiyo.


Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu idadi ya wanufaika wa mkopo ambapo amesema idadi ya kwenye jadweli inaonesha ni 78 na sio 1961 kama taarifa iliyotolewa na Wizara.


Nondo ameida kwamba kutokana na idadi ndogo ya vijana waliopata mikopo kwa awamu ya kwanza ni vema dirisha la awamu ya pili likafuguliwa ili litoe fursa kwa vijana wajitokeze kuomba Mikopo hiyo.


Hata hivyo ameshauri kuwa ili kuwezesha Vijana wengi kupata mikopo ni vyema baadhi ya vigezo viondolewe ikiwemo kuondoa kigezo cha leseni ya biashara kwani baadhi yao ndio kwanza wanaonba mikopo ili waanze kufanya biashara.


Ameendelea kufafanua kuwa takwimu ya wanufaika 78 wa mkopo aliyoitoa ni tofauti na iliyotangazwa  na Wizara husika,kwani Wizara ya Maendeleo ya vijana imetangaza kuwa vijana waliopata Mikopo ni 1961 kati ya 30384 walioomba.


Amesema kuwa idadi ya wanufaika 78 aliyoipata ni majina yao yaliyotajwa kwenye taarifa ya Wizara na idadi iliyoongezeka kufikia 1961 hajui imetoka wapi kwani hata yeye aliomba peke yake ingawa katika jedwali ameongezewa majina ya watu 10 ambao hajui wameingizwa vipi na hawatambui.


"Ni vyema Wizara ya Maendeleo ya Vijana itoe ufafanuzi hawa watu walioongezwa wametoka wapi ili kila kijana afahamu na kuondoa sintofahamu ya ongezejo hilo."amesema Nondo.


Halikadhalika ameiomba  Wizara hiyo kuelezea kwa kina sababu za vijana wengine kukosa Mikopo ili wafanye marekebisho katika zoezi la awamu ya pili la  uombaji wa Mikopo hiyo hatua itakayosaidia vijana wengi kupata mikopo.


Pia ameshauri kuwa fedha zilizopelekwa Wizara za kisekta ni yvema zikarejeshwa katika Wizara ya Maendeleo ya Vijana ili itoe fursa kwa Vijana wengi kupata mikopo tofauti na ilivyo sasa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3