Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAKONGORO NYERERE ASHINDA KWENDA WORLD CUP CANADA NA CRDB BENK

MAKONGORO NYERERE ASHINDA KWENDA WORLD CUP CANADA NA CRDB BENK

 

Na Matukio DaimaMedia 


Kupitia droo kubwa ya FIFA World Cup 2026 fainali Mpango na Tembo Card inayochezeshwa na CRDB Benk mtoto Hayatt Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere ameibuka mshindi wa kwenda kuangalia fainal za kombe la dunia nchini Canada.


Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro amepigiwa simu mubashara na mtoa huduma wa Crdb bank baada ya kushinda, kupitia Card ya Visa Tembo anayotumia kwa matumizi ya fedha.


Makongoro amepewa taarifa ya kuwa ameshinda droo ya kwenda nchini Canada kuangalia fainali za kombe la Dunia 2026, akiongozana na wenzake wawili walioshinda tunzo hiyo.


CRDB imechezesha droo ya pili ya kusaka washindi wa kwenda Marekani,Canada na Mexico kuangalia mashindano ya fainali za kombe la Dunia, mashindano makubwa zaidi ya soka kwa timu za Taifa Duniani.


Kampeni hiyo imepewa jina la FIFA World Cup 2026'Fainali ndio mpango na Tembo Card visa 'ambapo imepata washindi watatu wa Tv Janja nchi 85,na washindi watatu walioshinda kwenda Canada.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3