TASAC, TRCS WATOA ELIMU YA UOKOAJI ZIWA TANGANYIKA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kwa kushirikiana na Shirika la uwakala wa meli nchini (TASAC) wameendesha zoezi maalum la utoaji elimu ya uokoaji na usalama majini kwa wakazi wanaozunguka mwambao wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuhusu namna ya kujikinga na ajali pamoja na hatua za kuchukua wakati wa dharura majini.
Zoezi hilo lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya mwambao wa ziwa hilo, lililenga kutoa elimu kwa wavuvi, wasafirishaji wa abiria pamoja na wananchi wanaotumia usafiri wa majini kuhusu namna ya kujikinga na ajali pamoja na hatua za kuchukua wakati wa dharura majini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Afisa Mfawidhi TASAC mkoa kigoma,Adam Mamilo TASAC alieleza kuwa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya uokoaji ikiwemo maboya, jaketi za kuokoa maisha na namna ya kutoa taarifa za ni muhimu katika kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za majini.


