Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
IRINGA MWENYEJI MAADHIMISHO YA 29 WIKO YA MAZIWA NCHINI

IRINGA MWENYEJI MAADHIMISHO YA 29 WIKO YA MAZIWA NCHINI



Na Berdina Majinge, 

Matukio Daima Media.

Wakati Mkoa wa Iringa ukiadhimisha wiki ya maziwa nchini Mkoa huo umeishukuru serikali kwa kuleta mradi mkubwa wa mageuzi ya tasnia ya maziwa na mabadiriko ya tabianchi (C-SDTP) ambao unatekelezwa katika Halmshauri za Wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufundi.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maadhimisho ya 29 ya wiki ya maziwa nchini yatakayofanyika Mkoani Iringa.

Kheri alisema kuwa Maadhimisho hayo yameandaliwa na Bodi ya Maziwa Tanzania chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mbadiriko ya Tabianchi (C-SDTP) pamoja na wadau mbalimbali wa Tasnia ya Maziwa nchini.


Alisema kuwa mradi huo ambao umekusudiwa kuongeza uzalishaji na kuboresha mnyororo wa thamani wa maziwa, utajikita zaidi kusaidia na kuendeleza maudhui ya BBT, kununua na kugawa ng'ombe bora wa maziwa, ujenzi wa miundombinu itakayowezesha ufugaji bora.

Ujenzi na ukarabari wa miundombinu ya kukusanyia maziwa, kupanua soko la maziwa kuanzisha bima ya mifugo,na kuwataka wana Iringa kutumie fursa hiyo, kukamata fursa ili kuongeza uzalishaji, ukusanyaji, uchakatiji wa maziwa, kuongeza pato la kaya na kuchangia kwenye pato la taifa.


“Lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha Urasimishaji wa Tasnia ya Maziwa, Uwekezaji, matumizi ya maziwa bora na salama ili kulinda afya ya mlaji, kukuza biashara rasmi ya maziwa na kuhakikisha Tasnia ya Maziwa inaongeza mchongo wake katika maendeleo ya uchumi wa taifa”alisema Kheri


Kwa mwaka huu 2026, maadhimisho yanaongozwa na kauli mbiu isemayo


 "Rasimisha Biashara ya Maziwa, Okoa Maisha ya Walaji, Ongeza Kipato, Changia Uchumi."

“Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha wadau wote wa tasnia ya maziwa kuendesha shughuli zao katika mfumo rasmi unaotambulika kisheria, kuhakikisha maziwa yanayozalishwa, kusafirishwa na kuuzwa yanakuwa salama kwa matumizi ya binadamu, kuongeza kipato kwa wafugaji na wafanyabiashara wa maziwa pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa”alisema.

Aidha aliongeza kuwa katika kipindi chote cha maadhimisho, shughuli mbalimbali zitafanyika zikiwemo,maonesho ya huduma na bidhaa za wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa,usajili wa wadau wote wa maziwa,Kuhamasisha uwekezaji katika uzalishaji, ukusanyaji, usafirishaji na usindikaji wa maziwa.

Pia kutakuwa na kongamano la wadau wa maziwa litakalowakutanisha wafugaji, wachakataji, wadau wa maendeleo, wasambazaji, wawekezaji na wataalam mbalimbali,utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya maziwa bora na salama,huduma za usajili wa wadau wa Tasnia ya Maziwa.

Aliongeza kuwa kutakuwa na mafunzo ya usindikaji maziwa, ufugaji wa kibiashara, lishe ya mifugo, uzalishaji na ufugaji unaokabiliana na mabadiriko ya tabianchi, kampeni za kuhamasisha unywaji wa maziwa shuleni na katika vituo vyenye Watoto wenye mahitaji maalum.

“Tasnia ya Maziwa ina mchango mkubwa katika lishe, ajira na uchumi wa wananchi wetu. 

Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika juhudi za kuimarisha sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa letu”alisema


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3