Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
DKT. MWIGULU ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA RAIS RUTO

DKT. MWIGULU ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA RAIS RUTO


Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba jana Mei 11, 2026 alishiriki chakula cha jioni cha kitaifa kilichoandaliwa na Rais wa Kenya Dkt. William Ruto kwa heshima ya Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa


Dkt. Mwigulu yupo nchini Kenya akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ushirikiano wa Afrika na Ufaransa (Africa Forward: Africa–France Partnership for Innovation and Growth Summit) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Lengo la mkutano huo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, teknolojia, nishati, afya, Akili Unde (AI), kilimo, uchumi wa buluu pamoja na viwanda.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3