DKT. KIGWANGALLA AAMSHA SHANGWE BUNGENI, BAJETI YA MCHENGERWA
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, ambaye ni mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni za HK Group, na Mdau wa Maendeleo nchini, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameamsha shangwe bungeni kwa kupigiwa makofi mengi na Wabunge baada ya utambulisho wake kama mgeni wa heshima (V.I.P) wa Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Mbali na kuhudumu kwenye Wizara ya Afya kama Naibu Waziri, na Mbunge kwa miaka 15, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye chama na serikali, ikiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Kamari za TAMISEMI na Huduma za Jamii, na pia MNEC.
Baadhi ya Madaktari wanaofanya kazi na washirika wa Maendeleo hapa nchini ambao walisoma pamoja na Dkt. Kigwangalla walijumuika pamoja katika tukio hilo Bungeni.
Awali Mhe.Mchengerwa ameweza kuwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambapo ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha jumla ya shilingi Trilioni 1.8 katika mwaka wa fedha 2026/27,
Mhe. Mchengerwa amesema kupatika kwa bajeti hiyo kutasaidia kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwemo vipaumbele vyote 11 ambavyo vimelenga kuiweka Tanzania kuwa mfano kwa utoaji bora wa huduma za afya kwa Wananchi Barani Afrika
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
