Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KAMPUNI YA KITANZANIA YA IZO MOTORS  YAZINDUA BETRI MPYA

KAMPUNI YA KITANZANIA YA IZO MOTORS YAZINDUA BETRI MPYA


Na Matukio DaimaMedia

Katika kukuza Sekta ya biashara nchini Kampuni ya kitanzania ya Izo Motors Ltd imekuja na bidhaa mpya "Izo Battery" yenye ubora wa hali ya juu kwa matumizi ya aina mbalimbali ya magari zinazozalishwa nchini humo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuubwa Kampuni hiyo Izo Mahenge  amesema kuwa ujio wa bidhaa hiyo umeleta manufaa makubwa katika mnyororo wa thamani ambapo zaidi wa wafanyakazi 60 na Mawakala 70 ambao wameungwanishwa katika mtandao huo.

Mahenga amesema kuwa, kwa sasa wanazo aina mbalimbali za betri katika size tofauti zinazokidhi mahitaji ya magari ya aina mbalimbali ambapo bidhaa hizo zinapatikana kwa bei nafuu kwa wateja wa jumla na reja reja.

Amesema kuwa katika kuhakikisha wanawafikia watanzania wengi zaidi kampuni hiyo imejipanga kutoa huduma ya usambazaji wa bidhaa hiyo Tanzania nzima, mijini na Vijijini kwa urahisi na haraka na uhakika kulingana na mahitaji ya mteja.



Kwa upande wake, Balozi wa Kampuni hiyo Dotto Magari amewataka wadau , wafanyabiashara , madereva , taasisi mbalimbali pamoja wananchi wote kutembelea ofisi zao na kujionea unora wa bidhaa na huduma zao.

"Izo Battery zinazalishwa hapa Tanzania,ni betri bora na imara,watumiaji wa magari wazitumie "Izo Battery" hawatajuta kuzitumia popote walipo."Amesema Magari

Nakuongeza kuwa"kwenye kiwanda chetu tumeajiri watu wengi sana zaidi ya watu 60,tuna mawakala zaidi ya 70 nchi nzima,wote wanasambaza hizi betri,tumekuja na vitu vya tofauti.

Amesema kuwa, Kampuni hiyo ipo jijini Dar es Salaam, Kariakoo katika mitaa ya Narung'ombe na Lumumba ambapo wateja watapata huduma bora bidhaa zenye viwango vya ubora pamoja na ushauri sahihi kuhusu matumizi ya betri na matairi .

 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3