Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
AL - MALLID WAIYANGUKIA SERIKALI

AL - MALLID WAIYANGUKIA SERIKALI

 .

Na Matukio DaimaMedia 

Taasisi ya kidini ya Al-Mallid imeiomba Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mwigulu Nchemba kupitia upya nyaraka mbalimbali zinazoonyesha umiliki halali wa kiwanja namba 8 kitalu A kilichopo Nzuguni Jijini Dodoma

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Taifa wa taasisi ya Al-Mallid,Yusufu Mikidadi amesema eneo hilo ni mali yao lengo ikiwa ni kujenga chuo cha Afya na nyumba za wafanyaka, ambao watahudumu katika hospital hiyo .


 "Kujengwa kwa Chuo cha Afya, hospital, nyumba za wafanyakazi itasaidia sana kuongeza ajira kwa watanzania, eneo hili la zaidi ya hekari 45 bado ni mali yetu kwani tumeshalipia Kodi zote zinazohitajika na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na nyaraka zinazoonyesha kuwa sisi ni wamiliki halali wa eneo hili"


Amesema mara baada ya kutokea kwa mgogoro wa umiliki wa eneo hilo  walimwandikia barua waziri mkuu bila kijibiwa ambapo waliandika tena barua Mwezi March 2026 mwaka huu huku wakiamini watapewa majibu stahiki juu ya eneo hilo ambalo wamepanga kujenga Kituo cha afya,hospitali na nyumba za watumishi ambapo watanzania watanufaika na mradi huo


Naye, Mwanaharakati Ahmed Kombo amesema licha ya taasisi hiyo kulipia ardhi hiyo lakini bado hawajapata fursa ya kukabidhiwa kwani walitumia sadaka za waumini wa dini ya kiislamu ili kupata eneo hilo.


Kombo, amemuomba Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kufuatilia suala hilo kwa kusikiliza pande zote mbili ikiwemo taasisi hiyo na wizara yake  ili kulipatia ufumbuzi suala hilo kwani linahusisha kundi kubwa la watu.


"tunakuomba kwa utulivu Mheshimiwa waziri wa Ardhi kuwaita watu hawa pamoja na kuwasikiliza na pia tunamuomba waziri mkuu wa Tanzania tukiamini hili suala liko kwenye uwezo wake na siyo la Mheshimiwa Rais"amesema Kombo.


Kwa upande wake, Mwanaharakati huru Joseph Yona ambaye aliambatana na viongozi wa taasisi hiyo ametoa wito na Ushauri kwa Serikali kushughulikia suala la mgogoro huo na kuikabidhi taaisisi ya Al-Malid eneo lake ili ianze kufanya uwekezaji.


"Mimi siwezi nikailazimisha Serikali ila ninaiomba ishughulikie suala hilo kwa kuwakabidhi ili mradi utakaotengenezwa uwanufaishe watanzania"amesema Yona.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3