Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO KAGERA WATAKIWA KUCHUKUA TAADHARI SIKUKUU

WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO KAGERA WATAKIWA KUCHUKUA TAADHARI SIKUKUU

 


Na Anold Deogratias Matukioa Daima Media Kagera

Kuelekea sikukuu ya pasaka waendesha vyombo vya moto mkoani Kagera wametakiwa kuchukuwa taahadhari wakati wanaendesha vyombo vyao hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuilika.

Wito huo umetolewa na kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kagera mrakibu mwandamizi Joseph Ngonyani wakati akizungumza na vyombo vya habari, ambapo amewataka madereva kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria za usalama barabarani kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu siku za sikukuu hivyo kuongeza hatari ya kutokea ajali.


“niwatake madereva kuchukua taahari wawapo barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuilika wawe makini lakini pia wakague vyombo vyao kama viko salama kabla ya kuanza kuviendesha ili kujiepusha na matatizo”

Aidha Kamanda Ngonyani amesema kuwa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kagera lipo tayari na limejipanga kuwahudumia wananchi kwa kufanya shughuli za uokozi katika sikukuu hasa katika maeneo ya fukwe na maeneo ya balaa ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao wanakuwa salama.

“tuko tayari na tumejipanga kuwahudumia wananchi tutapita maeneo ya fukwe hata kwenye balaa ili kutoa msaada pale itakapo hitajika ili kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao”

Pia mkuu huyo wa jeshi  la zima moto na uokoaji amewataka wananchi kutoa taarifa za majanga yanayohitaji uokozi kwa kupiga ya namba ya dharura ya 114, ili kupata msaada lakini pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi wahudumu wa kitengo watakapo maeneo yao.

“niendelee kuwakumbusha wananchi wa mkoa wa Kagera endapo kutakuwa na matukio yoyote ya moto au uokozi wasisite kuwasiliana na jeshi la zima moto na uokoaji kwa kutumia namba ya dharura 114 ili kupata msaada, na niwatake watu wasitumia namba hii kwa kutoa taarifa za uongo au kwa utani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”

Na baadhi ya wananchi mjini Bukoba akiwemo Johanes Mtalemwa na Odiro Trentin wamesema kuwa wamejipanga vyema kusherekea sikukuu ya pasaka kwa amani na utulivu na kukaa na familia zao au kufanya matembezi sehemu salama.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3