SABABU ZA VIJANA KUTUMIA VILEVI
NA EASTER KAMETA (UoI)
MATUKIO DAIMA
Baadhi ya vijana mkoani Iringa waeleza sababu zinazopelekea baadhi ya vijana kutumia vinywaji vyenye vilevi huku wakitaja kuwa ni njia moja wapo ya kupunguza msongo wa mawazo.
Upendo sapari ambaye ni mkazi wa semtema amezungumza na Matukio Daima na kusema kuwa vijana wengi hutumia vilevi kutokana na msongo wa mawazo huku akitaja baadhi ya sababu ambazo zinawafanya vijana wengi kuwa na hali hii na kudaikuwa ukosefu wa ajira ni chanzo.
"Msongo wa mawazo hufanya vijana wengi Kujiingiza katika ulevi hali hii hutokana na changamoto kama ukosefu wa ajira, matatizo ya familia, au shinikizo la maisha hivyo hupelekea baadhi yao kuanza matumizi ya vilevi huku wakidhani kuwa ni njia sahihi ya kutuliza au kukimbia matatizo."
Aidha kwa upande wake Patson Benard ameeleza kuwa baadhi ya vijana hufuata ushawishi wa marafiki huku akitaja kuwa vijana wengine wanapoona rafiki zao wanatumia vilevi hivyo hufanya na wao kutamani kufanya majaribio ya kutumia vilevi .
"Ushawishi wa marafiki Kama kundi la marafiki wanao tumia vilevi, ni rahisi kwa kijana kujiunga ili ajisikie anakubalika au asiwe tofauti na wengine pia udadisi na majaribio kwa baadhi ya vijana huanza kwa kutaka tu kujaribu kujua vilevi vina athari gani pale wanapo ona vijana wenzao wanavitumia ambao ni kundi lika nao hivyo hupelekea na wao kuiga na kuanza matumizi ya vilevi."
Vilevile Diana Reonard mkazi wa kihesa ameeleza kuwa vijana wengi hawana elimu juu ya madhara yanayotokana na utumiaji wa vinywaji vyenye vilevi pia ametaja kuwa wengine hutumia vilevi kwasababu ya matatizo ya akili na kihisia wakidai ni njia ya kujifariji ambapo si sahihi.
" Vijana wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya vilevi na wengine hawajui madhara ya muda mrefu ya vilevi, hivyo huanza bila kuelewa hatari na wengine hutumia vilevi katika matatizo ya kihisia au afya ya akili katika hali kama huzuni, upweke, au hata magonjwa ya akili vijana wengi huamini matumizi ya vilevi kama njia ya kujifariji."
Pia shadrack Jumanne ametaja kuwa upatikanaji rahisi wa vilevi katika mazingira yanayo zunguka vijana ni chachu ya wao kufanya matumizi hayo pia ametaja kuwa baadhi ya vijana huiga mifano mibaya kutoka kwa wanaowazunguka na wengine katika mitandao ya kijamiii.
" Upatikanaji rahisi wa vilevi Kama pombe au dawa za kulevya katika mazingira wanayo patiakana vijana matumizi ya vilevi huwa ni rahisi kuanza pia kuiga mifano mibaya kutoka kwa watu wanaowazunguka au wanaowaona kwenye mitandao ya kijamii wanaotumia vilevi na hupelekea vijana wanaweza kuona ni jambo la kawaida."
