Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MWIGULU ATAKA USHIRIKIANO WA KIKANDA NCHI ZA MAZIWA MAKUU  KUKUZA BIASHARA

MWIGULU ATAKA USHIRIKIANO WA KIKANDA NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUKUZA BIASHARA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Dk.Mwigulu Nchemba amezitaka nchi za ukanda wa maziwa makuu na ziwa Tanganyika kuinarisha ushirikiano wa kikanda ili rasilimalinzilizopo kwenye maeneo hayo zinufaishe nchi hizo na wananchi wake.

Mwigulu alisema hayo akifungua kongamano la biashara na uwekezaji kwa nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika lililofanyika April 16 mkoani Kigoma na kubainisha kuwa eneo hilo lina madini adhimu ambayo hayapatikani sehemu nyingine duniani.


Alisema kuwa kwa sasa dunia inaelekea kwenye matumizi ya madini hayo hivyo nchi za ukanda wa maziwa makuu hazina budi kuimarisha  ushirikiano na usalama  baina yao ili rasilimali na madini hayo yaweze kuchochea uchumi na biashara kwa wananchi wake

Waziri Mkuu alisema kuwa mkoa Kigoma kupitia bandari ya Kigoma imekuwa lango kuu la biashara kwa nchi za maziwa makuu na hivyo serikali imedhamiria kuweka mazingira ambayo yatachochea biashara na uwekezaji ikiwemo kuimarisha miundo mbinu  reli na usafirishaji majini ili biashara inayofanyika iwe na tija kubwa

Kupitia kongamano hilo Waziri Mkuu ameitaka  Mamlaka ya biashara ya nchini  (TANTRADE)  kufanya  utafiti wa biashara na masoko na kuona namna utafiti huo unavyoweza kuchochea biashara na uwekezaji kwa mkoa Kigoma ambao unarasilimali na fursa za biashara na uwekezaji ambazo hazijatumika.


Aidha Waziri Mkuu Ncheemba amewataka viongozi na watendaji wa nchii za ukanda wa maziwa makuu kuimarisha usalama na Amani katika nchi zao kwani Amani na usalama ndiyo msingi wa shughuli zote za uchumi na biashara zinazofanyika.

Awali  Waziri wa  Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa Alisema kuwa sekta ya uchukuzi imekuwa na mchango mkubwa katika usafirishaji wa mizigo na abiria katika kuongeza mnyororo wa thamani hivyo  serikali imejizatiti kuhakikisha inaimarisha miundo mbinu ya usafirishaji inayounganisha mkoa Kigoma na nchii za ukanda wa maziwa makuu ikiwemo reli iendayo kasi na  kuboresha bandari ya Kigoma.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3