Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HALMASHAURI ZATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA YA MSINDIKIZAJI WA MJAMZITO

HALMASHAURI ZATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA YA MSINDIKIZAJI WA MJAMZITO

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


HALMASHAURI za mkoa Kigoma kupitia idara za afya za halmashauri hizo zimetakiwa kuimarisha mpango wa  Mama wajawazito kuwa na wasindikizaji ili kuchochea jamii kwenda kwenye vituo rasmi vya kutoa huduma za afya unapofika wakati wa  kujifungua.


Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma, Nice Msendo alisema hayo wakati Shirika lisilo la kiserikali la thamani uhai likifunga mradi wa Mama msindikizaji ambao ulitekelezwa mkoani Kigoma kuanzia mwaka 2007  na sasa mpango huo unaachwa kuendelezwa na serikali.


Msendo alisema kuwa wadau wa maendeleo katika sekta ya afya mkoa Kigoma wamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia huduma za afya ikiwemo masuala ya afya ya mama mjamzito na watoto na majukumu ambayo ni ya serikali hivyo miradi kama hiyo inapofikia mwisho ni lazima waganga wakuu wa wilaya na timu za huduma za afya za mkoa na wilaya kuiendeleza.


Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Thamini Uhai, Dk.Banzi Msumi alisema kuwa  Mradi ulianza ukiwa na vituo tisa  na kwa sasa vipo vituo 149 vinavotekeleza huduma ya mama msindikizaji.

Dk.Banzi alisema mradi huo umemaliz muda wake ukiwa na mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua akitoa ushuhuda   wa Mama wajawazito 26,000 kwa mwaka jana kuijifungua vituo vya kutoa huduma huku   wakiwa na wasindikizaji.

 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3