Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAOMBI YAKUTANISHA FAMILIA NA CHADEMA NYUMBANI KWA LISU, IKUNGI

MAOMBI YAKUTANISHA FAMILIA NA CHADEMA NYUMBANI KWA LISU, IKUNGI

 

‎Ikungi, Singida

‎Wakati Mwenyekiti wa Taifa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lisu, akiwa mahabusu kujibu shitaka la uhaini, familia kwa kushirikiana na CHADEMA mkoa, na Kanisa Katoliki, Parokia ya Ikungi, umefanya ibada maalumu nyumbani kwake katika Kijiji cha Mahambe, kata Unyahati, tarafa na wilaya ya Ikungi mkoani Singida, kumwombea kwa Mungu kiongozi huyo.

‎Kaka yake Tundu, Muro Lisu, amesema leo aprili 21, 2026 kuwa, Misa kama hiyo hufanywa na familia na ukoo wa Lisu kila mwaka, itakuwa pia kumuombea kaka yao Alute Mughwai ambaye ni mgonjwa mkoani Arusha, na kuwaombea ndugu na jamaa wote, ambao ni marehemu.

‎"Kwa pamoja tumeshirikiana na Chama na Kanisa kufanya ibada hii muhimu kwa ajili ya ndugu yetu Tundu aliyepo mahabusu gerezani, kumuombea kaka yetu mgonjwa Alute, marehemu waliolala hapa, na kujiombea sisi wote ambao tupo hai hapa hii leo...', amesema Muro.


Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa Singida, Omari Athuman Toto, amesema misa hiyo ni muhimu kwa kiongozi wao aliyopo mahabusu kwa shitaka la uhaini, na kusanyiko hilo limewakutanisha viongozi ngazi mbalimbali wa chama, ikiwemo ngazi ya Kanda ya Kati, ngome ya wazee, vijana na wanawake.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3