HALI YA BIASHARA YA USAFIRI WA DALADALA MKOANI IRINGA
Baadhi ya madereva daladala Manispaa ya Iringa mjini,Wameeleza hali halisi ya biashara ya usafiri wa daladala kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta msimu huu,na kupelekea kupanda kwa nauli kwa baadhi ya vyombo vya usafiri.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Umoja wa madereva daladala Manispaa ya Iringa,Salimu Ngoda amesema kuwa hali ya biashara ya usafiri kwa daladala sasahivi wateja niwengi kutokana na kutokupanda kwa bei ya nauli, kwani bei yetu sisi ni elekezi kutoka Mamlaka husika.
Licha ya hivyo sisi kama madereva daladala hatujapandisha nauli ili kuwa rahisishia abilia wetu kusafiri kwa urahisi, pia halisi hii inasababisha daladala kuonekana chache kutokana na uwingi wa abilia ambao wana kwepa kupanda bajaji kutokana na kupanda kwa bei ya nauli.
"Tunaiomba Serikali yetu itusaidie kulinda daladala ambazo zinachukuwa bei rafiki kwa abili, ili hata mafuta yakipanda zaidi tuweze kuwa saidia abiria kusafiri maana bila hvyo abilia watashindwa kusafili kabisa kuelekea katika shughuli zao".
Huku Philipo Nyalusi mkazi wa Iringa,ambaye ni abilia amesema kuwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta kumepelekea hadi nauli kupanda, kwani tulizoea zamani nauli ya bajaji ni mia saba (700) lakini sasahivi ni elfu moja(1000) hali hii inakusanya kutumia bajeti kubwa kwa siku.
"Sisi kama abilia tunaomba serikali itusaidie kutoa bei elekezi za usafiri ili kuweka usawa, kwani tukiangalia wanaoumia sana ni wanafunzi wanashindwa kufika shule kutokana na bei ilivyo panda kwa kasi kikubwa upande wa bajaji".
Nae Neema Godfrey ambaye ni mwanafunzi amesema kuwa kwa sasa hivi sisi wanafunzi tunapata changamoto kubwa ya usafiri tunapoelekea shuleni kutokana na kupanda kwa bei ya nauli.
"Kutokana na bei ya usafiri inayotembea sasa, inapelekea wanafunzi kushindwa kufika shule na kusababisha kukosa kuhudhuria masomo na kurudi nyuma katika maendeleo ya kielimu, kutokana na hali tunazo kutananazo barabarani".
Tunaomba serikali itusaidie kutoa bei elekezi ya mafuta na naulii ili kuwasaidia madereva na abilia kujua bei halisi na kuweka sheria kali kwa watakao kiuka sheria zilizowekwa.

