DKT TUMAIN MSOWOYA AWATIA MOYO WANAWAKE KUTOKATA TAMAA
Apr 25, 2026
Mwanahabari na Mtumishi wa Mungu na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Dk Tumaini Msowoya ameshiriki na kutoa darasa katika kongamano la Wanawake wa Kikristo lililofanyika katika ukumbi wa Royal Palm, Mjini Iringa.
Kongamano hilo lililo andaliwa na Mchungaji Winnie Msami, kiongozi wa Kanisa la Living Water liliwakusanya mamia ya wanawake kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali kuhusu maisha na baadae maombi.
Msowoya aliwataka wanawake wasikubali kukata tamaa badala yake wakubali kujifunza mambo mapya kila siku.
"Elimu siku hizi ni nyingi, sio kama zamani. Tusiache kujifunza na marufuku kukata tamaa mpaka mkatisha tamaa afe. We can," amesema.


