Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CHUO CHA RDO CHATANGAZA FURSA YA MAFUNZO YA KOMPYUTA KWA VIJANA

CHUO CHA RDO CHATANGAZA FURSA YA MAFUNZO YA KOMPYUTA KWA VIJANA

Shirika la Rural Development Organization (RDO) lenye makao yake Mafinga, mkoani Iringa, limetangaza rasmi fursa ya mafunzo ya matumizi ya kompyuta (Computer Applications Course) kwa vijana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Mafunzo ya Ufundi Stadi wa shirika hilo, Bw. Obadia Ngailo, mafunzo hayo yatachukua muda wa miezi sita na yanatarajiwa kuanza tarehe 18 Mei 2026. Mafunzo yatatolewa katika vyuo vya RDO Mdabulo VTC, RDO Kilolo VTC na RDO Ibwanzi VTC.

Jumla ya vijana 25 watapata nafasi ya kushiriki katika mafunzo hayo, ambapo waombaji wote wenye uhitaji wanahimizwa kufika katika vyuo husika ili kujaza fomu za usajili. Aidha, wasichana na wanawake wanahamasishwa kujitokeza kwa wingi kwani watapewa kipaumbele katika upangaji wa nafasi.

Kwa upande wa gharama, washiriki watachangia kiasi cha shilingi 100,000 tu, huku gharama nyingine zikigharamikiwa na shirika hilo. Wanafunzi watakaofanikiwa kujiunga watapaswa kuja na mahitaji muhimu yakiwemo godoro la futi 2½, shuka na blanketi kutokana na hali ya baridi ya maeneo ya Mufindi na Kilolo, pamoja na vyombo vya chakula na vifaa vya kujifunzia.

Mbali na mafunzo, wanafunzi pia watapatiwa huduma ya chakula na malazi kwa kipindi chote watakachokuwa chuoni.

RDO imewataka vijana kutumia vyema fursa hii ili kujiongezea ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano, ambao ni muhimu katika soko la ajira la sasa.

kuwa kwa maelezo zaidi, wadau wanaweza kuwasiliana kupitia namba za simu +255 745 921 971 au +255 757 351 837, au barua pepe rdovetcoordinator@gmail.com.

l

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3