Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
JAMII YAASWA KUEPUKA MIGOGORO YA NDOA ILI KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI

JAMII YAASWA KUEPUKA MIGOGORO YA NDOA ILI KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI

 


Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Jamii mkoani Kagera imetakiwa kuepuka migogoro ya ndoa ndani ya familia ili kuimarisha malezi bora ya watoto na kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani, hatua itakayochangia ustawi wa jamii ya Wanakagera na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu katibu mkuu wa wizara ya Katiba na sheria Dkt.Fraklin Rwezimula wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa bodi za ndoa mkoani Kagera, ambapo alieleza kuwa migogoro ya ndoa imekuwa ikisababisha kutokuwepo kwa ustawi wa watoto pamoja kuchangia uwepo wa watoto wa mitaani.


“migogoro ya ndoa uathiri ustawi wa watoto na kuchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa watoto wa mitaani, kupoteza nguvu kazi na kuathiri maendeleo ya taifa hivyo kupelekea nchi kutofikia dira ya taifa ya 2025-2025”

Aidha Dkt. Rwezimula ametaka kuimarishwa kwa ndoa katika jamii kwa maslai mapana ya jamii na taifa kwa ujumla na hivyo kuwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa weledi katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha migogoro mingi ya ndoa inasuruhishwa na sio kwenda mahakamani kwa lengo la kupata talaka.


“nichukue nafasi hii kusisitiza kuwa wajumbe wa bodi si maakimu bali nyinyi ni wasuluhishi jukumu lenu si kutoa hukumu bali ni kutumia kila njia na mbinu zinazowezekana kusaidia na kuwezesha pande mbili kufikia muafaka kwa njia ya mazungumzo na mariadhiano”

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo wakili wa serikali Oscar Allan amesema kuwa bodi hizo zina jukumu kubwa la kuleta amani katika jamii kwa kusuruhisha migogoro ya ndoa ambayo kwa kiasi kikubwa ndio imekuwa chanzo cha migogoro mingine ikiwemo ya aridhi.

“bodi hizo zinajukumu kubwa hasa la kuleta amani na ustawi wa jamii kwa kutatua migogoro ya ndoa ambayo ndio chanzo cha migogoro mingine, hivyo ukiponya ndoa umeponya jamii  na taifa kwa ujumla”


Nao baadhi ya wajumbe wa bodi akiwemo Idrisa Murashani ameshukuru kwa kupewa mafunzo hayo na kueleza kuwa yamewaongezea uwelewa zaidi namna ya kusuruhisha migogoro ya ndoa.

“tunashukuru kwa mafunzo haya yametuongezea uwelewa zaidi namna ya kutatua migogoro ya ndoa na kutambua kuwa bodi za ndoa sio chombo cha kupita kwenda mahakamni kudai talaka bali ni chombo cha kusuruhisha migogoro na kujenga jamii imara”

Naye Midase Bakari amesema kuwa kwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuhakikisha jamii inawakuwa na amani kwa kusuruhisha migogoro na kubatilisha ndoa zisizokuwa halali kama za utotoni.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3