Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CCM BUKOBA YATAKA KUKAMILIKA KWA KITUO CHA MABASI

CCM BUKOBA YATAKA KUKAMILIKA KWA KITUO CHA MABASI

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Kamati ya utekelezaji ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM), Bukoba mjini mkoani Kagera imemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Bukoba kuukamilisha kwa wakati ili kurahisisha shughuli za usafiri na kukuza uchumi wa mji huo.


Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mji huo mwenyekiti wa CCM Bukoba mjini Muganyizi Zachwa amemtaka mkandarasi huyo kufuata matakwa ya mkaba wake kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati .

“tulikuwa tunahoji kwanini mkandarasi huyu alipewa miradi miwili ya stendi na soko lakini niliambiwa ulikubali mwenyewe na ukasema unauwezo wa kuitekeleza sasa pambana mheshimiwa mradi huu uishe kwa wakati au kama kuna tatizo la pesa tujue ila nimeambia fedha ipo inakuja ”

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho msimamizi wa mradi huo mhandisi Dickson Kissa amesema kuwa mradi huo umechelewa kutokana na changamoto ya uwepo wa mwamba katika eneo hilo ila kwa sasa wameanza zoezi la uchimbaji wa msingi.

“kilichotuchelewesha ni ulipuaji wa mwamba ila kwasasa tunaendelea na uchimbaji wa msingi na kwasasa mashine za ipo saiti baada ya kulipua mwamba tuligundua tunahitaji kulipua tena mwamba”


Naye katibu wa CCM, Bukoba mjini Shaban Mdoe amewataka wasimamizi wa mradi huo kutoa ajira za muda kwa wananchi wa kata ya Nyanga na majirani wa mradi huo ili na wao wanufaike na mradi huo na pia kuwa walinzi wa mradi na kuepukana na suala la wizi wa vifaa.

“shughuli amabazo haziitaji elimu na zinazohitaji elimu na qualification wanazo, watu wa kata hii ya Nyanga anza nao hao ilo ndio jambo la msingi mtapendwa na mtapewa ushirikiano wa kutosha, maeneo mengine ya saiti kunakuwa na wizi mdogo kwa sababu hawaoni manufaa ya moja kwa moja hawaoni wakiguswa na mradi”

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Salvatory Sebastin amesema kuwa kukamilikwa kwa kituo cha mabasi manispaa ya Bukoba italeta manufaa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa kukuza uchumi wao na kurahisisha shughuli za usafiri.

“tunatarajia sasa stendi hii italeta manufaa kwanza kwa wafanyabiashara wadogo wadogo mama ntilie, boda baoda na huduma nyingi zitapatikana kupitia stendi hii kwenye mazingira yetu”

Ujenzi wa kituo cha mabasi Bukoba ulianza kutekelezwa tangu mwezi Octobar mwaka 2025, ikiwa ni miongoni mwa miradi minne mikubwa inayotekelezwa manispaa ya Bukoba kwa gharama za zaidi ya shilingi bilioni 40 fedha kutoka benki ya dunia kupitia mradi wa uendelezaji miji Tanzania (TACTIC). 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3